Freedom in Christ, not a freedom to sin Galatians 5:13a.-b.

Galatians   •  Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 2 views
Notes
Transcript
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kaitika kitabu cha Wagalatia na imekuwa mzuri sana. Ni ajabu maaraifa unaweza kupata wakati unaingia kila neno ya kila sentenci ya kila mstari. Kusema ukweli ni kama sanduku la hazina na kila jumapili sisi tunaingia kupata votu hivi kutoka Mungu wetu. Si manneo yangu au maneno ya mwengine ni neno la Mungu wetu na ni yeye tumefika kuabudu leo. Wiki iliopita tulimaliza kuona Paulo kuwaambia wakristo wa galatia alijua walifundishawa vizuri na hawawezi kufuata hii uongo wa wapenda sheria au Judaizers. Waliingia kusema tohara ni lazima kufuata Yesu na kuwa wana wa Mungu. Tuliona Paulo kusema Hawa watu watachukua hukumu yao. Tumeona msalaba ya Yesu kristo ni kikwazo au shida kwa watu wingi sana hata leo, kwa sababu inatoa matendo yetu yote tunaweza kutenda kupata wokovu na inatuonyesha ni Yesu Kristo na kazi yake na maisha yake na kifo chake na ufufuo wake imetuleta wokovu na ni zawadi yeye anatupea kwa neema yake. hakuna kitu sisi tunaleta kwa meza ya wokovu wetu. Kusema ukweli ni kitu tunaleta ni dhambi zetu, ni chafu yetu na ni yeye anatusamehe na ni yeye anatusafisha. Tafadhali kumbuka Waefeso 2:8-9 mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Hii ni tamu sana, kwa sababu hakuna kitu ninaweza kuongeza na hakuna kitu ninaweza kutoa, ni ya Mungu na ni kamilifu. Wakati hawa walimu wa uongo walijaribu kuchafua hii Paulo alisema angependa sana wangejikata nafsi yao. Ni kali lakini si mchezo wakati watu wanajaribu kuongeza vitu kwa zawadi ya Mungu, na uona watu wanafanya ujinga wingi sana kufikiri wanasaidia Mungu na wokovu wao ni ajabu na inakasirisha watu ambao wanajua ukweli.
Kumbuka nimekuambia mara mingi ilestory ya watu kuua kuku halafu kuzungusha juu ya kichwa mara tatu kutoa dhambi zao. Sasa fikiria hii, umeweka kazi ya Yesu msalabani sawa sawa na mtu kuzungusha kuku juu ya kichwa chake? hii ni kufuru, ni blasphemy. na hakuna tofauti ya kitu cho chote tunajaribu kuongeza. Sisi tulikuwa chini ya hii uzito wakati tulikuwa wasioamini lakini sasa Yesu Kristo ameleta uhuru kwetu. Angalia mistari yetu ya leo: Wagalatia 5:13-15 Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombee, Baba wetu tunasema asante sana kwa hii nafasi leo kuingia hii nyumba pamoja na watu wako na kufungua neno lako, kweli ni hazina na umeandika kwa watu wako kujua wewe zaidi. Naomba utafungua macho yetu na masikio yetu kuona na kujua ukweli wako na kutoka hapa na kutii hii ukweli. Tunaomba hii yote katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, Amin.
Siku zetu kwa kila desturi, kwa kila rangi na kila nchi dunaini nzima kila mtu anataka uhuru zaidi. Wanataka uhuru kufanya kama wanataka. Kusema ukweli ni adui mbili ya uhuru wa kikristo ni uhalali na ulegevu au kwa kiingereza inaitwa license. Sisi tunataka kuchunga sana, hatutaki kuwa na uhalali na uhuru wetu na pia hatutaki kutumia vibaya. Shida ya siku zetu ni kama miaka elfu mingi ilioptia kwa kitabu cha waamuzi 17:6 Siku hizo hapakuwa na mfalme katika israeli; kila mtu alifanya hayo aliyoyaona kuwa ni mema machoni pake mwenyewe. angalia nje, angalia kwa news, tunaona hii kila mahali. Hata Amerikani tuko na wanaume wanasema hawa ni wanawake na wanawake wanasema hawa ni wanaume, hata watoto wanasema hawa ni paka. Wakati tunasahau Mungu, kila mtu anafany mema machoni pake na inaogoza sisi kuwa mahali tuko saa hii. Na wakati unaendelea na dhambi yo yote, ikiwa ni ulevi, ua kuema uongo au kupigana na watu au kuiba au tamaa za ngono dhambi yo yote unapoteza njia yako, na hii dhambi inakutumia. Yesu alisema kwa kitabu cha Yohana 8:34 nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. Wasioamini ni mtumwa kwa asili yake iliyoanguka. Yeye ni Mraibu (Addict) hana udhibiti wa mawazo na matendo yake. Kama mlevi, sisi sote tunajua mlevi, labda wewe ulikuwa mlevi zamani, unajua, kila fikirio ni kwa pombe, unatamani sana kuonja ile kinywaji, hata unaanza kupata pesa kununua, hata unasahau uko na famlia nyumbani, na zaidi na zaidi anakuwa mtumwa ya ile dhambi. Kila kitu unajaribu kufanya labda inafanya kwa muda, labda wiki moja, labda mwezi moja lakini unarudi kwa Bwana wako hii dhambi ni bwana wako na imekushika na unashindwa. Hii ni kila dhambi si ulevi peke yake.
Ni dawa moja ya uhuru kweli kweli na tunaona kwa Yohana 8:36 ‌Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. Hii ni ajabu na zawadi na ukweli wa Ukristo na ni mandhari ya kitabu cha Galatia ni Uhuru wetu katika Yesu Kristo. Ukristi ni Uhuru.
Mlango wa kwanza hadi hapa Paulo amepigana na Uhalali na hatari yake. Unakumbuka 5:1 Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa. Paulo aliogopa hawa watarudi chingi ya kongwa la utumwa wa sheria. Walikuwa na walimu amabo wanajaribu kufunza hawa kutii sheria kuliko kuamini Injili ya Yesu. Paulo alionya hawa kuchunga sana mtu yo yote anajaribu kutoa uhuru wao. Uhuru wao kutoka dhambi, hatia na laana ya torati.
Pia ni mzuri kukumbuka wakristo wa Galatia si wayahudi lakini ni mataifa. Hawa hawajakuwa na torati ya Mungu, hawajajua utaratibu wake na hii maeno yote. Uhuru wao ilikuwa tamu sana. Angalia mstari yetu Wagalatia 5:13a. ninyi, ndugu, mliitwa. Ninyi ulitiwa na Mungu mwenyewe kuingia ufalme wa Mwana wake si kwa utumwa wa kisheria lakini angalia Vs.13a. ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru. Kweli Kweli wayahudi walishangaa. Ukisoma agano la kale ni mambo mingi sana walitenda kumpendeza Mungu, maisha yao yote ilkuwa kufuata torati na wote walishindwa, kwa sababu hawawezi na walikuwa chini ya laana. Na Yesu aliingia na kumbuka Wagalatia 3:13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; alifanya hii naam na gani? Mathayo 5:17 Yesu alisema Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Hajashindwa na sasa kila mtu ambaye aliitwa kuwa watoto wake sisi tunaisha maisha yetu ndani yake na kwa sababu ya hii tuko na uhuru.
Sasa Uhuru ni nini hapa? Maana yake ni nini. Uhuru hapa ni wewe si chini ya torati na hii utaratubu wake kulazimisha wewe kusihi maisha yako naam na gani. Uhuru kutoka Sherehe za agano la kale, uhuru kutoka mfumo ambye hakuna mtu anaweza kufanya, uhuru ya kujua Mungu anakupokea kwa sababu ya Yesu na kazi yake si kazi yako ambaye haiwezsi kumpendeza Mungu. Uhuru kujua tumesafishwa, tuko safi kwa sababu ya yesu na tunasimama haki kwa sababu ametupea haki yake. Kwa wakristo kurudi kwa agano la kale na mila na kanuni yake ni kurudi chini ya uzito wake bure kabisa. Haiwezi kusaidia kwa sababu haijasaidia hawa. Ikiwa uko hapa leo au unajua mtu ambaye anajaribu kufuata torati tafadhali ni mzuri kushika, huwezi, hata hawa walishindwa. Hata kila mfalme wa wayahudi walishindwa, Hata makuhani wengi wao, walishindwa. Ni mzuri unajua Sheria ya serikali ya Agano la Kale ilifutwa kabisa katika Kristo. Kusudi la namna hiyo ya sheria lilikuwa kuwatenga Wayahudi kuwa watu wa pekee waliochaguliwa na Mungu na kuwazia dhabihu ya Masihi anayekuja, Kristo. Kristo alipokuja, alama za dhabihu yake zilikoma kuwa muhimu, kwa sababu dhabihu iliyokamilishwa na ya mwisho yenyewe ilifanywa kikamilifu na milele.
Sasa kwa sababu ya hii yote tuko na shida ingine na tunaona wengi siku zetu wanakimbia na hii adui ingine ya uhuru wa kikristo. ni ulegevu au license. Rudi kwa kitabu cha Galatia 5:13b. lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, Uhuru kutoka dhambi na nguvu yake juu yetu, si uhuru kuishi dhambini na kujipendeza. Wengi siku hizi watasema Bibilia haijasema, usifanya hii ama hii. Labda ni ukweli lakini ni mzuri kuuliza maswali, nikifanya hii kitu italeta sifa kwa Mungu, au nikifanya hii kitu inaweza kuleta shida badaye. Ninyi umesika mimi kusema mara mingi hapa kwamba kukunywa pombe si dhambi, na ni kweli, Bibilia inasema kulewa ni dhambi. Mimi ninaweza kunywa pombe lakini lazima ninajiuliza, nikikunywa pombe nitakuwa mfano gani, nikunywa pombe nitataka zaidi kesho au kesho kutwa, itaongoza mimi wapi? Hii mambo ya License au Uhuru wa kikristo ni lazima tunachunga sana. Wengi siku hizi wanapata tatoos, wanakunywa pombe, wanatumia lugha ambaye si mzuri sana, Musiki, nguo, chakula na mambo mingi sana. Shida ya sisi binadamu ni tabia yetu ya kuwa mwenye dhambi tutafuata tamaa za mwili mpaka inatuua. Kwangu mimi nitasema siwezi kucheza na vitu hivi kwa sababu ninajua mwisho yao inaniongoza wapi, na pia kwa watu amabao ni viongozi wa kanisa lazima tunajua watu wanaangalia sisi. Paulo alisema kwa kitabu waraka wa kwanza wakorintho 6:12 Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote. Sisi wakristo tuko na uhuru lakini si kila kitu ni halali kwetu.
Paulo anawaambia hawa wakristo wa galatia, ninyi unaweza kuenda njia ingine haraka, kwa sababu wewe si chini ya torati usifikiri unaweza kufanya kama unataka, usicheze na vitu ambavyo inaweza kuleat shida badaye. Usijipendeza, usijifurahisha na tamaa za mwili kwa sababu ya uhuru wako. Unaona kwa mstari yetu vs.13c. lakini uhuru wenu USIWE SABABU! Maana ya hii ni wakati unafungua maisha yako kwa vitu hivi unatoa nafasi, nafasi kwa huyu ya zamani, dhambi zako za zamani kuingia tena. Usiwe sababu ya hii mwili na tamaa zake, kutenda dhambi kama inataka. Uhuru wa kikirsto wetu haiwezi tumiwa naam na hiyo. Yesu Kristo hajaleta uhuru kwa watu wake ili wanaweza kufanya vitu ambavyo wanataka kufanya. lakini hii uhuru imeletwa kwetu ili tunaweza kufanya kama Mungu anataka sisi kufanya.
Swali nzuri kuuliza ni hii, kwa nini tunataka kurudi kwa ile chafu na taka taka baada ya Yesu ametuokoa kutoka vitu vile. Umeokolewa kutoka nini? Kwa nini utataka kurudi uko? Baada ya mtu anatoka gereza anataka kurudi ukweli? Kwa nini wakati sisi tumetolewa kutoka ufalme wa giza na tumewekwa kwa ufalme wa nuru tutarudi ukweli kwa ufalme wa giza? Yesu kristo alilipa kwa hii taka taka yote na maisha yake msalabani, si kwako kuendelea na hii chafu lakini sasa unaweza kuwa na uwezo ndani yake kuisho maisha tofauti. Petro alisema kwa waraka wa kwanza wa petro 2:16 kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu. Sisi tumekuwa kiumbe kipya, unakumbuka ile mstari. Waraka wa pili wakorintho 5:17 mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. Imeenda. Lakini nataka ninyi kujua walimu wa uongo wanapenda sana kutumia hii uhuru wa kikristo na kuchafu maana yake. Wanapenda kufundisha kwamba uko na uhuru katika Yesu, sasa unaweza kufanya kama unataka bila wasi wasi ya hukumu, bila kuogopa matokeo ya matendo yako. Hata wanasema watu wanaona bibilia tofauti, moja anasema maana ya hii mstari ni hii na mwengine anasema ni hii na wote wako sawa, kwa sababu ako ndani ya Yesu. Ni mzuri sisi tunajua kila msatri ya bibilia iko na mana moja, na ni neno la Mungu halafu ni maana yake, sisi hatuwezi kusema according to me, kwangu inamanisha hii. tulisoma Yuda jumapili ingine lakini ni mzuri sana tuangalia tena Yuda vs.4 Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema, na hii neno neema hapa inaweza kuwa uhuru Mungu ametupea, Wabadilio uhuru, neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo. Wanafanya hii kwa njia au tabia ya maisha yao na kama wanafundisha watu kufanya.
Paulo alwaambia wagalatia ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo. Wiki Ijayo Mungu akipenda tutaangalia maana ya Paulo kusema bali tumikianeni kwa upendo. Ni muhimu sana na tukiweza kufanya kama anasema tutauma uhuru wa kikristo wetu vizuri.
Leo asabuhi labda umesikia neno la Mungu na ukweli wake na labda umejipata hata wewe mwenyewe unajaribu kupata wokovu kwa matedno yako au labda unafikiri umeokoka kwa sababu ya tendo fulani unatenda, nitaomba sana tafadhali tubu kwa hii na weka imani yako katika Yesu Kristo na kazi yake. Ikiwa hujaweka imani yako katika Yesu naleo unatoka kuongea zaidi, labda uko na maswali, ongea na sisi baada ya ibada yetu, tuko hapa kusaidia.
Asanteni Sana, Bwana wetu yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more