The Flesh Pt.4

Galatians   •  Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 2 views
Notes
Transcript

Galatians 5:20-21a.

Leo asabuhi tunendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Wagalatia na tumefika Mlango wa tano vs.20. Kwa wiki mingi tumeona vita ambaye iko ndani ya sisi sote. Ni muhimu sana sisi sote tunashika kwamba tuko vitani. Na hii vita ni vita ya milele yetu. Pia ni vita kwa roho za watu, kila dakika, kila siku ya maisha haya. Hii si mchezo na matokeo yako na maana mingi sana baada ya kifo chetu. Hii ni sababu ni muhimu sana watu wanasikia ukweli wa neno la Mungu, kwa sababu hakuna kitu kiingine inaweza badilisha mtu. Ni kweli mimi ninweza kubadilisha tabia yako kwa sababu unafanya kazi hapa kwa mission na sisi tunasema huwezi kuwa mlevi na kulala na malaya au huwezi kulala na mtu ambaye si bwana ama bibi yako, tunataka wewe kuwa knaisani kila jumapili, na kwa sababu unfanya hapa unakubali. Hii ni tabia yako lakini moyo wako, mawazo yako si kitu ambachio siwezi badilisha, hii ni kazi ya Mungu. Kazi yetu hapa ni kupanda mbegu ya ukweli tunapata kwa neno la Mungu, au labda ni kuweka maji kwa ukweli umeshaa pata na kuonyesha wewe Mungu anasema nini, lakini ni Mungu ndiye anayesababisha ukuaji wa mbegu hiyo amabye imepandwa. Ni yeye anapea zawadi ya wokovu na ni yeye anapea zawadi ya imani yetu na Mungu anasema kwa kitabu cha Warumi 10:17 imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Ikiwa imani yako imetoka mahali yo yote ingine, kwa wimbo fulani au maneno ya pastor fulani au tendo fulani unatenda au kitu cho chote badala ya neno la Mungu, si imani ambaye inaleta wokovu kweli kweli. Bila watu kusikia ukweli wa neno la Mungu hakuna wokovu, hakuna mabadiliko na hii ni sababu unaona watu wengi ambao wanaenda knaisa kila jumapili maisha yao haijakuwa tofauti na wanafanya vitu ambavyo wasoamini wanafanya. Tukovitani, kwa roho za watu, kwa roho yetu, kwa ukweli wa neno la Mungu.
Kumbuka Paulo aliwaambia Wakristo wagalatia kuenenda na Roho wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Ni tamaa za mwili na Roho wa Mungu amabye anasihi ndani yetu wanapigana. Kwa wiki tatu tumeangalia matendo ya Mwili. Tumeona uasherati, uchafu na ufisadi na tumeona ibada ya sanamu na uchawi, Wiki iliopita tliona uadui, ugomvi na wivu. Ikiwa umekosa kuwa hapa tafadhali enda kwa kweli kweli ministry na angalia.
Tusome Mistari yetu kwa muktadha yao Kitabu cha Wagalatia 5:16-21 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Tuombe: Baba Mungu tunasema asante kwa nafasi hii ya leo kuingia na kushiriki pamoja kama watoto wako. Saidia sisi kukuabudu kwa ukweli, tusaidia udhaifu wetu na pale tunaposhindwa wewe. Wakati tunafumngua neno lako leo asabuhi fungua masiko na macho yetu, badilisha mawazo yetu. Mungu tunaataka kutii neno lako, tunaomba nguvu yako itusaidie. Tunaomba hii yote katika jina la Yesu. Amin.
Unaweza kuona kwa orodha ya Paulo anaendelea leo kuonyesha matendo ya mwili kwa uhusiano wetu pamoja na wengine. Wiki iliopita tulimaliza na wivu na tumeona wivu ni kali sana, kusema ukweli ni chanzo cha karibu kila kitu cha matendo ya mwili kwa uhusiano wetu na mwengine. Leo tutajaribu kumaliza hii sehemu ya matendo ya mwili kuhusu mahusiano yetu na wengine. Kumbuka Paulo alisema hii yote ni dhahiri, ni wazi kwa kila mtu kuona. Anaendelea kusema Hasira. Nani hapa anajua hasira ni nini? Nani hapa amekuwa na hasira? Hasira ni hatari sana. Inaleta shida mingi kwa watu. Mara mingi hasira inakuja kwa sababu ya majivuno ya mtu. Wivu inaleta pia kwa sababi mwengie anafaulu na inaksirisha mtu, ubinafsi inaleta hasira, hujaridhika na maisha yako. Mtu ambaye hana subira na hakuna kujizuia ni mtu ambaye anakasirika haraka. Kwa hii yote nitasema kwetu wakristo ni kukumbuka Bwana wetu Yesu kristo. Alikuwa kamilifu, hajatenda dhambi hata moja na watu walisema vitu vingi sana vibya kumhusu yeye. Watu wa uongi waliletwa mbele kutoa ushuhuda wa uongo juu yake na Bibilia inasema kwa hii yote tufuate nyayo zake Angalia Waraka wa kwanza wapetro 2:22-23 Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake. Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki. Ni ngumu sana. Sisi tunataka haki yeti wakati tumedhumuliwa (been wronged). Na wakati haifiki tunakasirika.
Tena ni mzuri kujua Bibilia ni wazi sana kuhusu mtu ambaye ni mtu ya hasira. Angalia Mithali 22:24-25 Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia nafsi yako mtego. Inasema usikuwa rafiki ya mtu ambaye ako na hasira nyingi. Utajileta shida nyingi sana. Kwa sababu hata wewe utaanza kujuaq njia zake na wewe utaanza kuwa mtu ya hasira. Ninakumbuka wakati nilikuwa kijana tulikuwa na rafiki ambaye alikasirika haraka. hata mtu anaangalia yeye vibaya ataenda kwa ulw mtu kusema, unaangalia nini? Na sasa wewe unsiama uko na yeye na unaweza kujipata unapigana na huyu mtu na rafiki zake kwa sababu rafiki yako ni mtu ya hasira. Hapa Kenya ni watu ambao wanasema UTANIONA. Ikiwa huyu ni rafiki yako bila shaka utajipata kwa shida. Kwa sababu ni mtu ambaye anafuata tamaa za mwili wake. Kinyume ya mtu wa hasira ni nini? Ni mtu ambaye mtu huleta amani. Uko na UTANIONA halafu uko na mtu amabye atasema tafadhali tunaweza kuketi na kuongea kuhusu hii shida. Natumaini unaona tofauti. Kanisa tafadhali usikuwe watu wa hasira italeta shida mingi kwako, kwa familia na kwa kanisa.
Kitu kiingine Paulo anasema kwa hii orodha ya matendo ya mwili kwa wagalatia 5:20 ni Fitina, Faraka, Uzushi. Vitu hivi vi tatu vinaenda pamoja. Lakini ni mzuri sisi hapa kwa Sekenani hatuna watu wa fitina, Faraka ba Uzushi nafikiri tunaweza kuruka Meneno haya! Hapa tumejaa sana na watu wa fitina. Iko kila mahali na iko kanisani zaidi. Kwa nini iko kanisani zaidi? kwa sababu kanisa limejaa na wasioamini. Ni watu ambao wanapenda dini kuliko Yesu, ni watu ambao wanapedna kufuata Pastor fulani kuliko Neno la Mungu. Fitina ni nini? Fitina ni mtu ambaye anajiangalia peke yake. Mahitaji yake ni muhimu zaidi ya kila kitu, na wakati hawezi kuopata kama yeye anataka anaanza kuleta shida kwa watu. Kwa sababu ya ubinafsi wao wanaleta uongo kuajribu kupata kama hawa walitaka. Ninyi unajua watu wa fitina? Ukiangalia kanisa ambalo iko na fujo mingi bila shaka utapata mtu wa fitina hapo. Yakobo 3:16 ya sema Maana hapo palipo wivu na ugomvi, hii ni neno letu fitina, ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. Paulo aliwaambia kanisa la Filipi kwa Wafilipi 2:3 Msitende neno lo lote kwa kushindana, hii ni neno letu tena fitina, wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Mtu wa fitina ni mtu ambaye ako na majivuno mingi sana. Na wakati uko na mtu wa fitina utakuwa mtu wa faraka. Utagawa watu. Utagawa kanisa, utagawa watu wa familia, shida kila wakatyi ukopamoja. Hapa kwa kanisa letu nataka kusema ninashukuru Mungu kwa sababu hatujakuwa na watu wengi wa fitina na faraka hapa. wamekuwa, bado wengine wako lakini bado ninyi umeendela kuonyesha hawa upendo na kuonyesha njia ya kweli, hamjatengana kwa sababu yao na hujakubali washinde. Lakini ikiwa wewe ni mtu wa tabia naam na hiyo ni mzuri unajua hii ni hatari sana kwako.
Mungu anasema kwa neno lake ni vitu yeye anachukia. Tunapata hii orodha kwa kitabu cha Mithali 6:16-19 Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. Nafikiri ikiwa tunasoma kitu kama hii tutataka kujua sana vitu hivi ni nini na sisi tukaa mbala sana. Uko tayari Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu. Umeona ile ya mwisho apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu. Mungu anachukia hii. Wakati wewe unasema kitu ambacho inaleta marafiki wanapotengana Mungu anachukia mtu kama hii. Unajua rafiki yako amsema hii, unajua rafiki yako amefanya hii, nimesikia rafiki yako. Chunga sana! Na sijui kwa nini hapa lakini ni kama watu hawa na maisha, wanaingia maisha ya watu wengine na wanajaribu kuharibu. Wewe Mkristo endelea na maisha yako ya kufuata Yesu na kupenda wengine kama nafsi yako.
Neno lingine tunaona kwa hii orodha ya Paulo ni Uzushi. Hii neno hapa inaenda pamoja na Fitina na Faraka. Hawa walimu wa uongo ambao wameingia kwa wagalatia wengi wamefuata hawa na mafundisho yao. Hii ni sababu Paulo alisema kwa Wagalatia 1:6 Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine. Bila shaka wametoka njia na wanafuata uongo. Lakini bila shaka ulikuwa na wengine hawajafuata hii uongo na wamekaa kwa ukweli. Hawa ambao wanafuata hii uongo wataleta uzushi, watataka kutengana na hawa ambao hawajafuata hii uongo. Sasa unaona njia imefungulia kuleta fitina na faraka kujaribu kufuza hawa au kuleta aibu kwa hawa wengine. Uzushi iko na uhai mingi sana kwa makanisa hata leo, kwa dunia nzima. una vikundi tofauti kanisani na utaona ni hawa wako pamoja na hawa wanaongea na wengine wanawachana nje. Uko na group moja wanapenda hii musiki na group ingine wanapenda musiki tofauti. Uko na group moja wanaoenda hii pastor na wengine wanapenda huyu assistant pastor. Na wanataka agenda zao ziwe juu ya wengine na wanaanza kupigana na kuahribu wengine an kuchafua jina lao. Tena natumaini sana unaona hatari ya hii. Sisi tumeitwa kuwa watoto wa Mungu, sisi sote ambao ni wakristo ni ndugu na dada. Zaburi 133:1 ya sema Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja. Kweli hakuna kitu kiingine kama wakristo wakuwa na umoja kanisani. Ni ushirika mtamu. Hii ni sababu Oaulo aliwaambia wakristo waefeso kwa kitabu cha Waefeso 4:2-3 kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. Shetani anapenda sana hawa watu wa fitina, faraka na uzushi kwa sababu wakati vitu hivi viko kanisani inaleta aibu kubwa kwa jina la Yesu. Ni kama wakristo wanafanya kama watu wa dunia.
Kwa mwisho tunaona neno liingine kwa orodha ya Paulo ansema Husuda. Hapa hii neno ni karibu sana wivu kusema ukweli ni moja lakini tofauti kidogo. Wivu ni wakati unatamani kitu cha mtu mwengine, lakini husuda ni wakati uko na chuki kwa sababu ya ufaulu wa mtu mwengine. Au kwa sababu watu wako na vitu na wewe huna uko na chuki kwa ule mtu. Sisi Wakristo hatuwezi kuwa na husuda bii ni tendo la mwili kabisa. Kama wivu husuda inaleta watu kufanya na kusema vitu vya maajabu. Kumbuka kama tulisoma kwa Yakobo alisema mahali hii iko ni machafuko na kila tendo baya. Hii itaharibiu mtu haraka sana. Mahali wivu na husuda inatoka si mzuri Hata Yakobi anatuambia hii onatoka wapi. Angalia Yakobo 3:14-15 Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli. Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani. Hii ni wazi. Ikiwa hii imekushika uko na shida mingi sana, hata zaidi ya mlevi.
Kanisa tafadhali ninaomba, tujipime kujua ikiwa sisi tunaishi kwa matendo ya mwili, ni hii mwili wetu inatuongoza au ni Roho ya Mungu. Ikiwa unaanguka mtihani ninaomba sana, tubu, ikiwa wewe si Mkristi ninaomba ukweke imani yako katika Yesu Kristo, hakun akitu au mtu mwengine anaweza kukutoa kutoak ufalme wa giza na chafu yake na tamaa zake. Yesu kristo anaweza kukupea maisha tofauti, unaweza kiumbe kipya. lakini ni lazima kuamini na kuwa na moyo na mawazo mpya. Iko hapa lep asabuhi. Ikiwa unataka kuongea zaidi tafadfhali ongea na sisi baada ya ibada yetu. Wiki ijayo Mungu akipenda tutamaliza hii orodha ya matendo ya mwili na tutaona matokeo kwa watu ambao wanaishi kwa mwili.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more